-->

VIDEO:Nasubiri Ripoti ya Wafanyakazi 9000 wa Serikali Wenye Vyeti ‘Feki’ – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati Jumamosi hii akizindua majengo ya Hosteli za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amefunguka kwa kusema kuwa anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya kufoji.

Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.

“Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi,” alisema Rais Magufuli

Aliongeza, “Kwa hiyo mnaweza kuona shida zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibia 19000, mikopo hewa, wanafunzi ambao walikuwa ni hewa ni zaidi ya 56000. Kila mahali unapoenda kuna tatizo lakini ni lazima tuyatatue haya matatizo kwa sababu mlinichagua kwaajili ya matatizo haya,”.

Rais amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii na kuiunga mkono serikali katika harakati za kuwaletea maendeleo watanzania wa chini.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364