-->

Wadau Wataka Ofisi ya Bodi ya Filamu Iwe Basata

Bodi-ya-filamu-Godfrey-Mngereza

Godfrey Mngereza

VIONGOZI wa vyama na mashirikisho mbalimbali ya sanaa wakishirikiana na wadau mbalimbali wameliomba Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kuipatia ofisi Bodi ya Filamu katika jengo la Baraza hilo ili kurahisisha utendaji wake.

Pia viongozi hao wameliomba Baraza hilo lirudishe ofisi za mashirikisho ya vyama vya sanaa katika jengo lake ili vyama hivyo viwe na ushirikiano wa karibu katika utendaji na kumrahisishia msanii anapotaka huduma za vyama na mashirikisho hayo.

Viongozi wa mashirikisho hayo ya sanaa kwa nyakati tofauti walisema kurudishwa kwa ofisi za mashirikisho hayo kutaleta uharaka wa utendaji kazi zinazohitaji mashirikisho hayo kuwa pamoja na pia kuleta ushawishi wa kutokuwa na mwingiliano wa kazi zote kufanywa na Baraza hilo.

“Kuna kazi za kuandikisha na kutoa vibali kwa wasanii kwenye kufanya maonyesho mbalimbali ya sanaa vinatolewa na Baraza la Sanaa moja kwa moja bila kupitia mashirikisho husika, hii inatokana na mambo mengi, lakini pia inachangiwa na ofisi za mashirikisho hayo kuwa mbali na ofisi za Baraza hilo, hivyo tunashauri ofisi za mashirikisho zirudishwe katika jengo la Baraza la Sanaa, Basata ili tufanye kazi kwa ukaribu,’’ alifafanua Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Disco nchini, Asanterabbi Mtaki.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza, alisema lengo la Bara za hilo ni kukamilisha uchaguzi wa viongozi wapya wa mashirikisho ya wasanii ili kuweka mfumo rasmi wa kuendesha sanaa kwa mafanikio.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364