-->

Bila Kujuana Bongo Kutoka ni Kazi- Mai

Maimuna-Salum

Mai mwigizaji wa Filamu

MSANII chipukizi wa Filamu Bongo Maimuna Salum ‘Mai’ amefunguka kwa kusema kuwa wasanii chipukizi kupata nafasi za kuigiza ni mtihani kwani bila kujuana na Muongozaji au mtayarishaji inakuwa si rahisi kupewa nafasi kucheza nafasi kubwa japo katika malipo napo kuna changamoto zake.

“Tunaipenda sanaa lakini kuna changamoto kubwa sana kwani kama hauna urafiki na Director au Producer inakuwa ni vigumu kuigiza hata kama una kipaji vipi, lakini hautakiwi kukataa tamaa,”anasema Mai.

Msanii huyo anasema kuwa bado hata kwa wale wanaopata nafasi bado wanaendelea kuwa chipukizi kwani hata suala la soko si nzuri hadi watayarishaji wanaingia katika madeni baada ya kukosa fedha kwa wakati, lakini changamoto nyingine watazamaji kununua filamu kwa kuangalia sura katika makava.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364