Hawa Wamebambwa Utamu!
WAUMINI wa dini ya Kiislam duniani wapo katika mfungo wa Mwezi wa Ramadhani. Mfungo huo ni moja kati ya nguzo tano za dini ya Kiislam, ikiwa ni nguzo ya nne.
Katika nguzo hii, waumini hujizuia kula na kunywa mchana kutwa, sambamba na kujipinda katika kutenda mambo mema na kuepuka maovu, huku pia wakiomba msamaha kwa Mola wao kwa matendo yote waliyofanya miezi 11 iliyopita.
Kwa waumini wanaojitambua na kufahamu umuhimu wa ibada hii, huwa hawafanyi utani, hutumia muda mwingi kuepuka machafu yote ambayo walikuwa wakiyatenda.
Hata baadhi ya mastaa nchini ambao ni waumini wa dini hiyo, hawapo nyuma katika kutekeleza ibada hiyo, wakibadili aina ya maisha waliyokuwa wakiishia siku za nyuma. Kuna walioachana na matumizi ya vilevi kwa sasa na wengine kutengana na wenza wao waliokuwa wakiishi nao kama mke na mume, ili tu kupata wasaa wa kujikita katika ibada hiyo ya mfungo wa Ramadhan.
Ingawa kwa mafundisho ya Kiislam vitendo vyote haramu vimekatazwa, lakini kwa kujishtukia mastaa hao wanaona ni vyema kutafuta fadhila za Mola wao kwa kuepuka baadhi ya dhambi.
Ndiyo maana wapo walioamua kuoa kabla ya kuingia mfungoni ili kupata fadhila, kwa wale ambao wameshindwa kuoa wamewatema kwa muda wenzao wao na Mwanaspoti linakuletea baadhi ya mastaa hao.
JUX NA VANESSA
Wawili hao ni wenza wa siku nyingi na kati ya mastaa wanaokimbiza kwenye fani ya sanaa. Jux yeye ni muumini wa Kiislam, majina yake kamili yakiwa ni Juma Mussa ‘Jux’, katika kuhakikisha avurugi funga yake imedaiwa kwa sasa ametengana kwa muda na Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ili kupisha mfungo wa Ramadhan.
HARMONIZE NA WOLPER
Wenza hawa wamekuwa gumzo kwa siku za karibuni, kutokana na penzi lao kumea ghafla kama uyoga. Harmonize staa kutoka Lebo ya Wasafi (WCB) anayejipenyeza kwa kasi kwenye Bongo Fleva ameangukia mikononi mwa mwigizaji nyota, Jacklyne Wolper.
Harmonize ni muumini wa Kiislam na majina yake kamili ni Rajab Abdulrahman, kwa sasa inadaiwa ameamua kujiweka kando na Wolper, ili kupisha mfungo, yaani mfungo umemnasa utamu wakati ndiyo kwanza penzi lake likichipukia.
Mwanaspoti
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA WEWE NI MFANYA BIASHARA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA