Wanadatisha: Wema Sepetu, Masogange, Sanchi, Kajala, Gigy Money
Baadhi yao kwa kutambua kuwa wameumbwa vema, hutumia fursa kujitosa kwenye fani ambazo zimekuwa zikiwatengenezea fedha, huku umaarufu wao ukizidi maradufu.
Mwanaspoti linakuletea wadada 10 wakali wanaodatisha mashabiki wao ndani na nje ya nchi kupitia sanaa ya muziki na filamu;
1-SANCHI
Huyu ni video vixen aliyejaliwa sura na umbile matata, kiasi cha kuwafanya waimbaji wa muziki wa kizazi kipya kujipanga foleni kugombea kumpa tenda za kupamba video za nyimbo zao. Nani hataki kumuona kwenye songi lake.
Majina yake kamili ni Janeikunda Rimoy a.k.a Sanchoka, ambaye licha ya kupamba video, lakini ni mwanamitindo na mjasiriamali anayemiliki kampuni yake ya Golden Eyes Traders. Kifupi mwanadada huyu anatetemesha.
2-MASOGANGE
Huyu ni kimwana anayekimbiza katika muziki akiwa ni mpamba video za wasanii mbalimbali ukiwamo uliompatia jina hilo la Masogange ulioimbwa na Belle 9.
Majina yake halisi ni Agnes Gerard na ni miongoni mwa warembo wanaodatisha vidume kutokana na kujaliwa na mvuto wa aina yake wa sura na maumbile.
Masogange ni mtamu kumuangalia kwenye video alizoshiriki kwani, anajua kuzitendea haki kamera, japo kwa sasa amepumzika kwa muda kwenye fani hiyo, hii ni kutokana na mishemishe zake na kesi inayomkabili.
3-WEMA SEPETU
Utasema nini kwa kisura huyo maarufu ndani na nje ya nchi? Wema Sepetu, Miss Tanzania wa mwaka 2006 ni mkali bwana. Mara baada ya kung’ara katika urembo alihamia kwenye filamu kwa msaada mkubwa wa aliyekuwa mpenziwe, Steven Kanumba.
Tangu hapo nyota yake imzeidi kung’ara na hii ni kutokana na kujaliwa umbile na sura matata inayochokoza, akiwa na kisauti fulani hivi cha kusisimua.
Wema ni kati ya mastaa wenye kutajwa kuwa na mashabiki wengi nchini na watu wanaofuatiliwa kila uchao kupitia mitandao ya kijamii.
4-GIGGY MONEY
Huyu ni mmoja ya waimbaji wa muziki wanaokuja juu kwa sasa, japo alianzia kama mpamba video za muziki (Video Queens). Giggy ni mtata kwelikweli kwani, kutokana na kujaliwa umbile kike amekuwa akijiachia atakavyo na kuwa kivutio kwa mashabiki wa kiume. Kwa sasa mwanadada huyo ambaye pia ni mtangazaji anatamba na ngoma yake iitwayo ‘Nampa Papa’, japo huko nyuma alitatamba na ‘Tikisa Supu’ na nyingine.
5-SHILOLE
Mwimbaji wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ a.k.a Shishi Baby, ni miongoni mwa wasanii waliojaliwa mvuto wa sura na umbo. Shilole, anayetokea Igunga, Tabora ni mwimbaji wa miduara na mwigizaji wa filamu za Kibongo.
Mvuto wa sura yake na kujichanganya kwake kisanii kumemfanya awe mmoja ya wasichana wanaodatisha Bongo.
6-KAJALA MASANJA
Mwigizaji wa filamu za Bongo Movie, Kajala Masanja ni miongoni mwa wale wanaodatisha kwa mvuto wa sura na umbo. Kajala, ambaye mbali na kujishughulisha na filamu, lakini ni mjasiriamali na kwa sasa ni Balozi wa Kampuni ya kubeti nchini. Mvuto wake umewafanya wanaume wengi kutokwa udenda kwa mama huyo wa mtoto mmoja wa kike.
Alianzia kwenye urembo kabla ya kuibukia kwenye fani ya uigizaji wa filamu. Irene Uwoya ni mrembo bwana, kwani ana sura na umbile linalodatisha, kiasi sio ajabu Hamad Ndikumana ‘Kataut’ beki wa zamani wa Rwanda kumfungia safari kuja kumuoa miaka kadhaa iliyopita.
Uigizaji wake wa mahaba mazito umewafanya mabazazi kutokwa mate, naye amekuwa akitumia fursa kisanii kupita fedha kwa filamu zake na zile anazoshirikishwa zinanunulika mno mradi sura yake iwemo. Itafute Oprah aliyocheza na kina Kanumba na Ray ndio utajua Irene ni mwanadada wa aina gani. Anadatisha bwana!
8-SNURA MUSHI
Msanii huyu wa muziki na filamu naye hajambo. Mashabiki wake wamempa jina la Chura litokanalo na ngoma yake, yenye jina hilo iliyokuwa ikionyesha wadada na hata yeye namna mzigo unavyotetemeka, yaani tentenete.
Snura ana mvuto bwana na anajua kujiachia kwenye kazi zake iwe kwenye filamu ama muziki akiwa jukwaani ama videoni.
Amejaliwa mvuto wa sura na umbile na pia kipaji cha sanaa anacho na sio kama anabahatisha kama baadhi ya wasanii wengi wa kike nchini. Wacha adatishe kwani nini bana.
9-SKAINA
Kwa sasa amekuwa kimya sana, lakini mwigizaji huyo Skyner Ally ‘Skaina’ acha kabisa, kwani ni mvuto wake wa sura na umbile limemfanya adatishe mashabiki.
Skaina mtamu bwana, walioziona filamu alizocheza akiibuliwa na Ray wa Kigosi ama video ya Kimbiji ya Bob Junior ndio wanaujua namaanisha nini?
Mwigizaji huyo amejaliwa mvuto wa sura, umbo na rangi yenye kuita na kufanya mashabiki hasa wa kiume kuvutiwa na kazi zake, japo kwa sasa anapiga mishemishe zake kibao za kusaka noti kama mjasiriamali.
10-FLORA MVUNGI
Mwimbaji na mwigizaji huyu aliyekuwa mke wa mkali wa Takeu, H-Baba naye wamo bwana. Amejaliwa sura mwanana na macho ya kuita huku akiwa na umbile matata kwelikweli. Kila anapopita jirani yako, basi ni lazima shingo itapinda kiaina.
Amekuwa akifanya vizuri zaidi kwenye filamu kabla ya kujitosa kwenye muziki akitoa nyimbo kadhaa aliolewa na H Baba na kubadili dini na jina akiitwa Khadija a.k.a H-Mama. Kwa sasa anaonekana kuwa kimya kidogo tofauti na zamani wakati akicheza filamu mbalimbali, lakini inaelezwa kuwa amepumzika kidogo kwa majukumu ya kifamilia.