Wapo Wanaojiuza Kweli Bongo Movie- Rose Ndauka
Msanii wa filamu nchini Rose Ndauka amefunguka na kuweka wazi kuwa kwenye tasnia hiyo wapo baadhi ya watu wachache ambao wameingia kwenye tasnia hiyo wakiwa na lengo la kujiuza na kupata wanaume, ambao wamekuwa wakiichafua tasnia hiyo.
Kupitia kipindi cha Mkasi, Rose Ndauka aliweka sawa kuwa kuna wasanii ambao wanaingia kwenye tasnia hiyo kuwa kuwa wana vipaji na wanataka kufanya filamu kama kazi na kusema wapo baadhi ambao kweli wameingia kwenye filamu ili kupata wanaume au mabwana kupitia tasnia hiyo.
“Kiukweli si kila msanii anayeingia kwenye filamu anataka kupata wanaume japo wapo baadhi ya watu wanasukumwa na hiyo hali lakini ukweli ni kwamba wapo wasanii ambao wanaingia kwenye filamu sababu wana vipaji na wanataka kufanya filamu kama kazi na kufanikiwa kimaisha” alisema Rose Ndauka.
Mbali na hilo msanii huyo alisisitiza kuwa kitendo cha wanawake kujiuza ni si kwenye tasnia ya filamu tu hata katika maisha ya kawaida watu hao wapo hivyo amedai hali hiyo ni hulka ya mtu mwenyewe na si kutokana na kazi anayofanya au kwa kuwa yupo kwenye filamu kama ambavyo watu wanadhani.
eatv.tv