-->

Prof Jay Afunguka Haya Kuhusu Mwana FA, Nikki Wa Pili, Roma Kuwa Viongozi

Mbunge wa Mikumi ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Prof Jay’ amewataja wasanii ambao wana uwezo wa kuwa viongozi kama wakipewa nafasi na wananchi.

Prof-Jay

“Wasanii wengi wana misimamo mizuri,wana shule lakini nina wasiwasi kama watakuwa na uwezo wa kujitoa kama hivi maana kazi ya ubunge si tu kuona na kutaka kuwa kama fulani,wangapi wanataka kuwafanyika kazi wananchi, lakini wengi nimeona mwelekeo wao ni mzuri kwasababu maandishi yanazungumza mtu anachokiimba unasikia filling zake na unaona ni mtu wa aina gani Kama Roma, Kala Jeremiah, wana misimamo ambayo inaweza kufanya kitu kuwasaidia watu” Alisema Joseph Haule.

“Lakini pia MwanaFA na Nikki Wa Pili wako kwenye msimamo huo kwa sababu kuna kitu kipo ndani yao lakini bado wanaficha hawataki kukitoa ni kama Prof Jay alivyokuwa akikificha zamani nilikuwa nina uwezo wa kuongoza lakini nilikuwa nashindwa kuamini kama naweza kuongoza kwahiyo watu kama hao wakiamini wanacho hicho kitu na kuthubutu kufanya kile kitu kwa watu wakaomba ridhaa naamini wanaweza wakawa viongozi” Aliongeza Joseph Haule.

Cloudsfm.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364