-->

Wasanii Zaidi ya 70 Wajitokeza Usaili wa Filamu

ZAIDI ya wasanii wa kike na mastaa wa filamu Bongo 70 wenye umri kati ya miaka 16 na 30, wamejitokeza katika usaili wa filamu mpya ya ‘Xballer’ uliofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

irene paul

Irene Paul

Aliyeongoza zoezi zima la usaili huo ni prodyuza na mwigizaji mkuu katika filamu ya ‘Going Bongo’, Ernest Napoleon ambaye kupitia filamu hiyo ameshinda tuzo ya filamu bora ya East Africa katika tuzo za filamu za nchi za Jahazi (ZIFF).

usail

Zoezi la usaili huo lilianza saa 5:00 asubuhi na liliendelea hadi usiku kutokana na idadi kubwa ya wasichana waliojitokeza ambapo kila mmoja alionyesha kipaji chake cha kuigiza kwa kadiri alivyoweza.
Waigizaji watakaochaguliwa katika usaili huo watashiriki katika filamu hiyo ambapo picha zake zitapigwa katika nchi ya Uingereza na Zanzibar.

“Unajua hapa nimeona vipaji vingi ingawa makosa ni kidogo sana ila nadhani kuna haja ya kuweka vipande hivi katika mitandao mbalimbali ili watu walioshindwa kufika kwenye usaili na wale wenye vipaji lakini wanahofu ya kuigiza waweze kujifunza kupitia humo,” alieleza Napoleon.

“Nimepanga kufanya usaili mwingine jijini Mwanza na kwingineko lakini itawezekana kama nitapata wafadhili maana hii sanaa ni ngumu lakini ili filamu iwe bora itabidi nitafute vipaji kokote Tanzania kwa kuwa filamu ni ya kimataifa na lengo lake ni kuuzwa duniani kote,” alisema Napoleon.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364