-->

Wengi Hawapo Tayari Kupiga Vita Dawa za Kulevya – Ray C

Msanii wa muziki wa bongo Fleva Rehema Chalamila kama Ray C amefunguka na kusema kuwa watu wengi hawapo tayari kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya nchini jambo ambalo linazidi kuwapoteza vijana wengi kutokana na matumizi ya dawa hizo.

RAYC90

Kupitia Account yake ya Instgram Ray C aliyasema haya na kuwataka vijana wa Tanzania kusimama mstari wa mbele kupiga vita matumizi ya dawa hizo kwani kuna watu wengi ambao hawapo tayari kuingia kwenye vita hiyo.

“Ifike hatua vijana na watanzania mpende maendeleo na kuelimisha jamii vitu vyenye tija kwa mustakabali wa taifa letu, wengine tumekuwa victim katika drugs and drug abuse ni matumaini yangu sasa watanzania wawe front line kusupport na kupiga vita madawa hayo. cha ajabu wengi wao hawako willing katika hilo Kwa hiyo vijana wenzangu nawaasa kupiga vita madawa ya kulevya Tanzania”. Alisema Ray C

Mbali na hilo msanii huyo alizidi kusema vijana wasipokuwa makini na wasipokuwa mstari wa mbele katika hilo nchi itazidi kupoteza nguvu kazi ya vijana ambao wengi wao wamejikuta wakitumbukia kwenye matumizi ya dawa hizo.

“Madawa yatamaliza kizazi bora cha watanzania ni wakati mwafaka kila mmoja wetu akachukua hatua kuanzia pale alipo, katika makazi yake ama mashuleni, maofisini, ama mashambani na mahosipitalini. Popote pale yatumikapo tuyapinge kwa nguvu zote.
Nashangazwa unapo poteza muda wako kupost wasted things katika Social Media kwamba fulani kasema hivi kafanya vile! You do this for the benefit” Aliuliza Ray C .

Akifafanua juu ya kazi yake ya muziki Ray C amesema licha ya kuendelea na dozi yake ya Methadone kwa sasa yupo katika maandalizi ya mwisho kuaanda nyimbo yake na kusema kuwa licha ya changamoto anazopata kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikimchafua tena ila anaamini kuwa atashinda na kufanikiwa na hawezi kurudishwa nyuma.

“Mimi niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaandaa nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone. Hujuma hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana na dawa za kulevya nchini mimi na taasisi yangu nitaendelea kusonga mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa”. Alisema Ray C.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364