-->

Wastara Akiri Sadifa Juma Kumharibu Kisaikolojia

STAA mahiri wa Bongo Muvi, Wastara Juma ameibuka na kusema aliyekuwa mume wake wa tatu ambaye ni Mbunge wa Donge, Sadifa Juma, amemuharibu sana kisaikolojia kiasi kwamba anamchukia kila mwanaume anayemweleza kuwa anampenda.

Wastara Juma na Sadifa Juma siku ya harusi yake

Akizungumza na Za Motomoto News, Wastara alisema kuwa huwa hataki hata kuiona kabisa picha ya mbunge huyo, iwe kwenye gazeti, televisheni au mtandaoni, kwani anahisi anamchukia kupita kiasi.
“Yaani Sadifa kaniharibu kisaikolijia, amenifanya niwaogope wanaume kama ukoma na nimetokea kumchukia, hata nimuone kwenye mitandao ya kijamii au gazetini nachanganyikiwa kwa hasira maana sitaki kumuona kabisa kwenye macho yangu,” alisema Wastara.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364