Wastara Amchimba Mkwara Mpenzi Wake, Bond
Msanii wa bongo movie Wastara amemchana mpenzi wake wa sasa Bond kwamba asipojirekebisha baadhi ya tabia zake atamuacha na akimwacha hatarudi tena kwake.
Hata hivyo Wastara amesema anaweza kuvumilia shida anazopata kwa Bond lakini anaweza kumuacha muda wowote kwani hahitaji ‘stress’ za kimapenzi huku akiweka wazi kuwa amejitahidi na amefanikiwa kumrekebisha kwa 80 % na endapo ataendelea na mambo yake ya zamani zamani ataachana naye.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Wastara amesema “Niseme tu ukweli kwamba kwa Sajuki hakuna mtu anayeweza kufikia upendo wetu kwa kuwa Sajuki alikuwa anajali kila kitu ambacho nilikuwa nakipenda, kitu ambacho mpaka sasa sijapata ni mtu ambaye amefikia hatua za Sajuki “. Alisema Wastara.
eatv.tv