Wastara Kufunga Ndoa Kisiri Kabla ya Ramadhani
Katika hali ya Kushitukiza inasemekana kuwa staa wa Bongo Movies Wastara Juma ana mipango ya kufunga ndoa siku za usoni kabla ya Ramadhani.
Mtu wa karibu wa Wastara Juma ambaye Hakutaka jina lake litajwe alimthibitishia muandishi wa footprinttz kuwa ni kweli Wastara anatarajia kuolewa.
” Ni Kweli Wastara anafunga Ndoa Siku Si Nyingi Ila huwa hapendi kuweka Mambo hadharani ” mtu huyo alieleza.
Aliongeza kuwa Wastara Amewaonyesha Pete ambayo ndio atavarishwa na Mwanaume wa sasa ambayo thamani yake ni Dola za Kimarekani 3,000.
Alipoulizwa kuhusiana na huyo mume mpya wa wastara haklutaka kuweka wazi ila alibainisha kuwa ni msanii wa bongo movie.
Juhudi za mwandishi kumtafuta Wastara ili alizungumzie hili ziligonga mwamba baada simu kutopokelewa.
Wastara ni moja kati ya mastaa wakubwa katika tasnia ya filamu hapa Bongo ameshawahi tutamba na filamu kadhaa kama Shayma, Mama na Mwana hapo nyuma na mwaka huu ameachia filamu ya Faulo.
Footprinttz Blog