-->

Wastara ‘Live’ na Aliyekataa Mahari Yake!

wastara (1) Wastara Juma na Juma Mbega ‘Masairo’.

WASTARA Juma ambaye alikataa mahari ya shilingi milioni tano ya kijana Juma Mbega ‘Masairo’, hivi karibuni walionekana laivu katika picha za pozi tofauti walizopiga sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.

wastara (2)Chanzo kilichovujisha picha hizo, kinasema licha ya mahari hiyo kukataliwa, lakini wawili hao hivi sasa ni kama kumbikumbi, kwani huonekana pamoja kila wanapokwenda, tena wakitumia gari la muigizaji huyo.

Inadaiwa kuwa wawili hao awali walikuwa wakiishi nyumba moja, enzi za uhai wa marehemu mume wa Wastara, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambaye alikuwa ni rafiki yake, hivyo kijana huyo kuwa kama shemeji wa muigizaji huyo.

Inadaiwa katika ukaribu wao wa sasa, wawili hao wamekuwa wakikesha studio, ambako Juma anarekodi singo yake ya muziki.

Gazeti hili lilimtafuta Wastara, ambaye alikiri kuwa karibu na kijana huyo, lakini akidai anafanya hivyo kwa vile ni kama shemeji yake ambaye ameishi naye kwa muda mrefu.

wastara (3)“Jamani yule mimi ni kama shemeji yangu, wala hakuna kitu kingine kati yetu na hakuna chochote cha zaidi katika ukaribu huo,” alisema.

Kwa upande wake, Juma alisema Wastara ni mtu anayemsaidia katika mambo mengi, lakini pia amemsogeza karibu ili kumfanya awe na furaha na kutowapa watu nafasi ya kumchezea.

“Sitaki kupinga kuwa Wastara ni mtu muhimu sana kwangu, na sitaki kumpa nafasi mtu yeyote yule kumuumiza na kumkosesha furaha kwa sababu najua aliyekuwa akimpatia ni kaka yangu tu Sajuki,” alisema Juma.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364