Waandaaji wa filamu Zilikamatwa Wajisalimisha Bodi ya Filamu
Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo alipokuwa akifanya mahojiano na mmoja wa waandaaji wa Filamu nchini aliyekutwa na kadhia hiyo Bw. Akim Igembe kutoka Kampuni ya Akim Master Film baada ya Filamu yake ijulikanayo kwa jina la “Mapenzi Uchizi” bango lake lilikutwa sokoni likiwa na alama ya Uhakiki kutoka Bodi ya Filamu wakati ilikuwa bado haijahakikiwa na Bodi hiyo.
“Operesheni ya kukamata Filamu zilizoingizwa sokoni kinyume cha sheria ambayo ilimshirikisha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ki ukweli imekuwa ya mafanikio sana maana sasa wameanza kujileta wenyewe.”Alisema Fissoo
Aliongeza, “Wakati tunapitia fomu ya Uhakiki wa Filamu hii tulibaini kuwa ni moja kati ya kazi tulizozikamata kutokana na kuwa na alama ya uhakiki bila kupitia kwetu, tena ikiwa na daraja 18 wakati katika daraja hali la filamu hiyo inapaswa kuwa ni daraja 16,”
Katika hatua ngingine, Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Filamu Tanzania, Moses Mwanyilu amepongeza hatua iliyochukuliwa na Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kupitia waziri wake, Nape Nnauye katika kuhakikisha wanatokomeza waharamia na uuzaji wa kazi za wasanii bila kufuata utaratibu za kisheria zilizowekwa.
Bongo5