-->

Wastara Ndoa Tena!

Wastara341

BAHATI ILIYOJE! Baada ya hivi karibuni mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kutimiza miaka mitatu kaburini, staa wa filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kwamba anatarajia kuolewa tena kwani ameshapata chaguo sahihi.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko nyumbani kwao Tabata Barakuda jijini Dar, Wastara alisema wakati wa msiba wa mumewe aliweka nadhiri kwamba ataolewa baada ya miaka mitatu hivyo kwa sasa yuko tayari kuingia kwenye ndoa nyingine.

Alisema kuwa, ndani ya mwezi huu anatarajia kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu ya mguu na atakaporejea atakaa siku chache tu kabla ya kufunga pingu za maisha na mwanaume anayefanya kazi serikalini (jina ni siri yake kwa sasa).

“Nitaolewa hivi karibuni na atakayenioa ni mtu mkubwa tu serikalini, watu watamjua siku hiyo ya ndoa lakini tayari ameshafanya taratibu zote zinazotakiwa, nikirudi tu kutoka India ndoa inafungwa,” alisema Wastara.

Wastara ni mama wa watoto watatu, aliwahi kuolewa mara tatu ambapo kwa ndoa atakayofunga na kigogo huyo, itakuwa ni ya nne.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364