-->

Wastara wa Sajuki Anahitaji Shilingi Milioni 37 Akatibiwe

MSANII wa Bongo Movie, Wastara Issa, anahitaji msaada wa kiasi cha Sh 37 mil ili akapatiwe matibabu nchini India, lakini mpaka sasa hakuna hata msanii mwenzake aliyekwenda kumjulia hali.

Wastara alikuwa mke wa marehemu, Sajuki Juma aliyefariki miaka mitano iliyopita kutokana na tatizo la mfuko wa chakula na alikuwa pia ni muigizaji.

Amesema, anahitaji kiasi hicho cha pesa kwa ajili kwenda kufanya matibabu ya mguu, mgongo na kichwa vinavyomsumbua.

“Mpaka nimeamua kutoka kwa watu na kuzungumza suala hili, nina shida na nimebanwa. Nahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali ili niweze kuokoa maisha yangu,”anasema Wastara.

Akizungumzia kuhusu wasanii wenzake kama wanajitokeza kumsaidia, Wastara anasema: “Hakuna hata mmoja, ninapowapigia simu wananipa pole tu, lakini kitu ambacho kinaniuma basi wangekuja hapa nyumbani hata kunijulia hali nione nina wenzangu, lakini imekuwa kimya.”

Wastara ametoa namba zake za simu kwa mtu yeyote aliyeguswa na ugonjwa wake, atume mchango wake kupitia namba 0768666113 kwa jina la Wastara Issa.

Chanzo:Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364