-->

Watayarishaji wa Muziki Bongo Wana Hali Mbaya Sana – Master J

Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Tanzania, Master J amesema watayarishaji wa muziki wa Bongo wana hali mbaya sana kwa sasa.

Master-J

Master J amejiwekea heshima kubwa kwenye;muziki wa Bongo Fleva, pia amefanikiwa kuwatambulisha wakongwe kibao wa muziki wa Bongo Fleva na Hip Hop ambao wamejiwekea heshima kubwa kwa sasa nchini.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Master J alisema ‘watayarishaji wa muziki Bongo wanahalimbaya sana’.

“Unajua maproducer wanahali mbaya sana sasa, madirector ndiyo wanamiliki magari na majumba. Kama inawezekana wasanii waende kufanya show mikoani na video zao halafu waone itakuwaje,” aliongezea.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364