Watu 32 Wafariki Katika Ajali ya Basi Karatu
Ajali mbaya imetokea Karatu Arusha katika mlima Rhotia baada ya basi dogo la St Lucky ya Arusha aina ya Coaster lililokuwa limebeba wanafunzi kutumbukia kwenye korongo na kusadikiwa kusababisha vifo kwa wanafunzi kadhaa.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ajali hiyo imetokea baada ya basi hilo kuacha njia na kuingia katika bonde la mto Mlera ambapo maiti wamepelekwa katika Hospital ya Lutheran Karatu.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa kati ya maiti hizo miongoni mwao wapo waalimu ni 2 dereva 1 na wanafunzi 29 ambapo wanafunzi wa kiume 11 na wasichana 18 nakufanya jumla yao kuwa maiti 32.