Watu Wamejifunza Kutoka Kwangu – Matonya
Matonya ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kuwa yeye kama msanii kuna mambo mengi ambayo watu huiga kutoka kwake, kutokana na ushawishi mkubwa alionao kwa jamii.
“Unajua tumebarikiwa na nguvu, tuna upendo mkubwa sana kwa watu kiukweli lazima tujue ndio maana kila ninachokifanya najitahidi kiwe kizuri kwa jamii, sipendi kufanya vitu vibaya, Mungu anisaidie, manaake tunaona kabisa watu wanajifunza vitu vingi kutoka kwetu”, alisema Matonya.
Pamoja na hayo Matonya amesema yeye kama binadamu wa kawaida pia anapenda sana kuongeza marafiki, kwani ndio wanaomsaidia katika mambo yake, na pia anaamini bado wanasuport kazi zake.
“Napenda sana kuongeza marafiki kwa njia njema, kwa hiyo naamini kabisa wote niko nao na wanaendelea kumsapoti matonya mpaka leo”, alisema Matonya.
Eatv.tv