Waziri Nape Azifungia Radio 5 na Magic FM Kwa Muda Usiojulikana
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, ametangaza kuvifungia vituo vya Radio 5 Arusha na Magic Fm Dar kwa muda usiojulikana kwa kosa la uchochezi.\
Waziri Nape amesema ameielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuvisikiliza kwa kina kisha kumshauri juu ya hatua zaidi za kuchukua.
Aliongeza kuwa kimsingi radio zote mbili kwa pamoja zimetangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake.
“Sisi kama Serikali tunatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani, umoja, mshikamano kwa kuwa ni muhimu sana. Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo Agosti 29, 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake” Amesema Waziri Nape.