-->

Wema Atumia Zaidi ya Milioni Moja Kutengeneza Nywele Zake kwa Wiki

Staa wa bongo Fleva, Wema Isaack Sepetu, ameweka wazi kwamba hutumia shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza nywele zake kwa wiki moja.

WEMA7321

Pia hutumia Sh 30,000 ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Hata hivyo, Wema aliliambia MTANZANIA kwamba si kila wakati hutumia kiasi hicho cha fedha, bali hutegemeana na aina ya nywele anazotengeneza.

Alifafanua zaidi kwamba gharama hizo pia zinatokana na kutumia ‘weaving original’ lakini wakati mwingine hutumia hadi laki moja na nusu kwa nywele za kawaida kama rasta.

“Huwa nabadilisha nywele kila baada ya wiki ambapo siku nyingine natumia milioni moja, siku nyingine laki saba au tano kwa sababu sipendi kukaa na nywele muda mrefu na nywele zangu ni ‘orijino’,” alisema.

Wema aliongeza kwamba anachopenda zaidi kwake ni kuwa na muonekano mzuri wa urembo kwa kuwa urembo upo kwenye damu yake.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364