-->

Wema Anatutoa Shimoni – Aunty Ezekiel

Msanii wa filamu bongo Aunty Ezekiel, amejivunia kitendo cha msanii mwenzake ambaye pia ni rafiki yake mkubwa Wema Sepetu, kuzindua filamu ya Heaven Sent kwa aina ya kipekee, na kusema huenda likawa tumaini jipya kwa bongo movie.

Wema Sepetu na Aunty Ezekiel

Akizungumza kwenye uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa sinema jijini Dar es salaam, Aunty Ezekiel amesema anaamini Wema amekuja kubadilisha tasnia ya filamu na kuwatoa shimoni wasanii hao, ambao walikuwa wanaanza kupotea kwa kukaa kimya kwa muda mrefu bila kazi mpya sokoni.

“Nimekuja kumuunga mkono Wema Sepetu ambaye amekuja na filamu mpya, naamini amekuja kuibadilisha tasnia ya filamu, labda amekuja kututoa tulipo shimoni na kutuleta juu”, alisema Aunty Ezekiel.

Aunty Ezekiel aliendelea kwa kusema ….”kwa njia moja au nyingine imeleta ‘bongo movie’ mpya, kwa muda mrefu hakujawahi kutokea kitu kama hiki, unapoingia tu hapa unaona kabisa tasnia ya filamu inaenda kubadilika, kwa hiyo ni kitu ambacho kinanipa faraja kama msanii”, aliseme muigizaji huyo.

Siku ya Jumamosi tar 26 Agosti 2017, Wema Sepetu amezindua filamu yake ya ‘Heaven Sent’ ambayo ilihudhuriwa na watu maarufu mbalimbli, wakiwemo waigizaji wa filamu za bongo na wa muziki pia.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364