Wema Awacharukia Ali Kiba, Diamond
MREMBO wa Bongo, aliye pia mwigizaji Wema Sepetu amewatolea povu waimbaji wa Bongofleva, Diamond na Ali Kiba kwa kuwaita ‘Wendawazimu’ na kuwataka wakue.
Wema alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa muvi yake katika ukumbi wa Mlimani City juzi, akisema waimbaji hao wanampa ugumu kwani anapenda kazi za Kiba na kazi za Diamond, lakini amachukizwa na bifu lao lisilo na maana.
“Kiba na Diamond ni wendawazimu, yaani wananiudhi sana, sema hawaelewi tu. Watu wanakuwa kama watoto wadogo kila siku mabifu tu, ifikie hatua wabadilike wakue sasa na sio mambo wanayoyafanya.
“Binafsi wananipa ugumu kwani mimi ni shabiki wao wote wawili narudia tena wananiudhi sana.”
Kiba na Diamond kwa sasa ndio habari ya mjini kwenye mitandao na mitaani kutokana na kutupiana maneno, baada ya Diamond kutoa wimbo wake unaoitwa Fresh Remix na katika wimbo huo kuna baadhi ya maneno ikiwemo neno la Cinderela ambapo watu wametafsiri kama ni dongo kwa Kiba.
Aidha juzi kati Kiba kaachia ngoma yake mpya ‘Seduce Me’ ulioibua vijineno kwa baadhi ya watu kuushabikia na kuuponda wimbo wa Fresh Remix. Hata hivyo, sasa Diamond na crew yake ya WBC wameachia ngoma ya ‘Zilipendwa’ iliyotoka sambamba na kazi ya Kiba.
Wimbo huo umeimbwa na wasanii saba akiwamo Rich Mavoko, Diamond, Rayvan, Lava Lava,Queen Darleen na Maromboso aliyekuwa Yamoto Band.
Mwanaspoti