-->

Msanii nguli wa filamu wa Marekani atua Serengeti

Arusha. Msanii wa filamu maarufu duniani na raia wa Marekani, Cynthia Rothrock, maarufu Lady Dragon, ametua kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Cynthia aliyewahi kushinda tuzo tano za filamu duniani kupitia filamu zake za mapigano, amefikia katika hoteli ya Grumeti Serengeti inayomilikiwa na bilionea wa Marekani, Paul Tudor.

Msanii huyo ambaye ameigiza zaidi ya filamu 31, miongoni wa zilizompa umaarufu ni Lady Dragon Xtreme Fighter na Deadliest Art.

Tangu atue nchini juzi Agosti 26, picha zake zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii duniani.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa mchezaji maarufu wa Uingereza, David Backham, safari ya Cynthia ni ya mapumziko binafsi.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa karate, Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete, amesema umetokana na kazi kubwa ya Serikali, Tanapa na wadau wengine kuitangaza Serengeti.

Shelutete amesema wasanii wengine wengi wakubwa duniani wanatarajiwa kuingia nchini, kutalii kama ambavyo imetokea mwaka huu.

“Mwaka huu umekuwa mzuri katika utalii nchini, tumepata watalii wengi maarufu duniani, wakiwemo wachezaji mpira, wasanii wa filamu na viongozi wa kisiasa,” amesema.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364