-->

Wema Sepetu Afunguka kwa Mara ya Kwanza Tangu Atoke Rumande

Staa wa bongo movie, Wema Sepetu ametoa shukrani kwa watu wote waliokuwa naye bega kwa bega tangu ashikiliwe rumande kufuatia kutajwa kwenye orodha ya kwanza ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya watu wanaohusishwa na biashara ya matumizi ya dawa za kulevya.

Wema alitoka kwa dhamana ya shilingi milioni 5 wiki iliyopita baada ya kupandishwa kizimbani kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambako alisomewa mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na msokoto wa bangi.

“Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia,” ameandika kwenye Instagram.

“Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu. Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote,” aneongeza.

“Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana. Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu tunasema asanteni sana.”

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364