-->

Wema Sepetu ataja sifa za mwanaume anayemtaka

Msanii wa filamu, Wema Sepetu ameibuka na kudai kwamba yeye si mwanamke anayependa wanaume wenye uwezo mkubwa kama tuhuma dhidi yake zinavyoeleza.

“Mimi napenda mwanaume anayejielewa,mwenye upendo na mchapakazi, ikitokea ana fedha itakuwa imetokea,lakini si mwanamke ninayependa pesa kuliko utu na mapenzi ya kweli,”alijinadi Wema Sepetu na kuongeza;

“Unajua pesa sio kikwazo katika maisha yangu, kwa sababu najua kuitafuta hivyo siwezi kubweteka kwa kutaka mwanaume mwenye pesa, hilo kwangu halipo, ninachotaka awe na upendo na thamani kwangu awe mfariji na si maumivu.”

Hata hivyo, Wema alisema hatoacha kuomba kila kukicha Mwenyezi Mungu ampatie mwanaume mwenye sifa anazotaka ili roho yake isuuzike.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364