-->

Rais Magufuli Amchangia Wastara Sh15milioni

Rais John Magufuli na mkewe Janeth, leo wametoa msaada wa Sh15milioni kwa msanii wa filamu nchini, Wastara Juma anayetakiwa kwenda nchini India kwa matibabu.

Msanii huyo anahitaji Sh37milioni zitakazogharamia matibabu yake ya mguu na mgongo na alitakiwa kwenda India tangu mwaka jana, lakini imeshindikana kutokana na kukosa fedha.

Kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na Rais kimekabidhiwa kwa msanii huyo leo Januari 26, 2018 jijini Dar es Salaam na katibu wa Rais, Ngusa Samike.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Wastara kupitia mitandao ya jamii, aliandika waraka mrefu akiomba msaada wa kiasi hicho cha fedha kwa maelezo kuwa ametumia kila njia bila mafanikio.

Hivi karibuni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alimpatia msanii huyo Sh1milioni.

Mwananchi

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364