Wema Sepetu Kuachia Filamu ya Mil. 40 Leo
STAA ‘grade one’ kunako filamu Bongo, Wema Sepetu amewajibu watu wanaoendelea kumsema kuwa hajui kuigiza kwamba, wajaribu kutupia jicho la tatu kwenye filamu yake mpya ya Heaven Sent ambayo inatoka leo (Ijumaa) ikiwa imetengenezwa kwa gharama ya shilingi milioni 40.
Akizungumza na Ijumaa, Wema alisema kuwa ameamua kutumia kiasi kikubwa cha pesa ili filamu ionekane nzuri na yenye hadhi kwa sababu filamu nyingi Bongo zinakuwa mbaya kutokana na bajeti kuwa finyu.
“Naamini kila mmoja anaweza kujua uwezo wangu mkubwa niliopewa na Mungu kwa kuiangalia filamu yangu ya Heaven Sent, ndani ya filamu hiyo utanijua vizuri ni msanii au naleta longolongo na humo nimejitupa utafikiri sio Wema mimi,” alisema.
Chanzo:GPL