-->

Wolper Acharukia Wasanii Wenzake

Dar es Salaam: Staa mwenye kiwango cha juu Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe amefunguka kuwa, wasanii wengi waliopo kwenye tasnia ya filamu ni wanafiki na wanafuata mkumbo, hawako kiuhalisia.

Jacqueline Wolper Massawe

 

Akizungumza na Showbiz, wakati wa maandamano ya kupinga wizi wa kazi zao na uingizwaji na uuzwaji holela wa sinema za nje, Wolper alisema kuwa, wasanii wangekuwa na umoja wangeungana siku hiyo kwa ajili ya kujua hatima ya kazi zao wanazozifanya na zinazowaweka mjini, lakini kwa kuwa wengi ni wanafiki imeshindikana.
“Nachukizwa na unafiki Bongo Movi, kwa kweli unakera sana, hawako kiualisia ndiyo maana kufika tunapotaka ni ngumu sana,” alisema Wolper.

Chanzo:GPL

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364