-->

Simfahamu Nay wa Mitego – JB

Msanii Jacob Steven  JB’ amedai kutomfahamu Nay wa Mitego na kusema pamoja na kusikia sehemu mbali mbali za maneno ya kashfa kutoka kwa msanii huyo yeye bado anampenda japokuwa hamjui na wala hajawahi kusikiliza nyimbo zake.

Akilijibu swali la Mtangazaji wa eNewz Duwe Santana kuhusu jinsi alivyopokea kauli ya wasanii waliondamana kuitwa ‘Matahira’ JB amesema hajaisikia kauli hiyo na wala hamtambui msanii huyo hivyo yeye anamuachia tu Mungu.

Mwalimu wangu wa economic aliwahi kuniambia One man’s meat could be another man poison, kwahiyo kama wao wametuona sisi matahira sisi tunawashukuru sana. Mimi ni Mkristo sijafunzwa kutukana nimefunzwa kuwapenda watu  wote na kuwaheshimu”– JB alianza kufunguka

Tazama video hii kumsikia vizuri zaidi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364