-->

Wolper Afungukia Alivyondanganyika Kwenda Afrika Kusini

Msanii wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amesema alijikuta akidanganyika kwenda Afrika Kusini kwasababu alitaka akasomee Kiingereza, lugha anayoamini ni muhimu wake.

wolper23

Akiongea kwenye kipindi cha Take One, kinachoruka kupitia Clouds TV, Wolper amesema kuwa chuki zilizopo kwenye kiwanda cha filamu na tatizo la kutoijua lugha hiyo ndiyo sababu nyingine iliyomfanya akubali kumfuata mpenzi wake Mkongo Afrika Kusini.

“Ndiyo maana mimi mwenzangu nilikubali kudanganyika kwenda South Afrika kusoma kizungu,” alisema.

“Mimi mchaga napenda hela, ilikuwa siyo rahisi kukubali kwenda kusoma Afrika Kusini na kuacha sanaa yangu napata mwenyewe milioni nne au tano maisha yangu yanaenda. Lakini nimekubali kwenda kule kusoma lugha at least nivuke hatua niende sehemu nyingine kwa sababu wenzetu huku wana chuki na hakuna kitu kinachoendelea vitu vimefeli. Lakini vitu vikagoma, I am sure kwamba bado sijachelewa nitafanya, nitajitahidi nitafika kule ninapotaka kufika,” alisema Wolper.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364