-->

Kajala Amwanika Bwana Mpya!

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja juzikati alimwanika bwana’ke mpya, kufuatia kupigana kibuti na Mbongo Fleva, Quick Raca, Risasi linakujuza.

kajala-1

Kajala (picha ya kushoto) na mwamme anayedaiwa kuwa bwana wake mpya

Katika Pool Party ya staa mwenzao, Shilole, iliyofanyika katika uwanja wa ofisi ya BKT iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, Kajala alimtambulisha mwanaume huyo bila kumtaja jina, akisema ndiye mtu wake rasmi kwa sasa.

“Naona unanitolea macho na kunitamani muda mrefu na unavyopenda umbeya unataka kujua hawa nilionao ni kina nani, naomba ufahamu kuwa huyu ndiye mchumba wangu wa sasa, ndiyo maana unaniona niko naye,” alisema msanii huyo.

Kajala, ambaye pia alimuonya bwana’ke huyo kuwa makini na paparazi wetu, alithibitisha usemi huo baada ya kuondoka pamoja na mtu wake huyo katika viwanja hivyo kuelekea Coco Beach kabla ya baadaye kuonekana tena pamoja wakinywa kinywaji kimoja ndani ya Ukumbi wa Club Billicanas.

Kabla ya kuwa pamoja na Quick Raca, Kajala alikuwa na mumewe, Faraji Chambo ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani, Machi 2013 baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji pesa, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364