-->

Wolper asaidia wananchi wa Golani Kimara

 

WOLPER

“Kuanzia mwaka juzi nimekua na desturi ya kushirikiana na watu siku yangu muhimu ya kuzaliwa
Mwaka juzi nilipata nafasi ya kukaa na watoto yatima na mwaka jana kituo cha wazee
Mwaka huu nimeamua kugusa maisha ya watu wengi zaidi
Kwahivyo kwa kutafakari jinsi gani tatizo la maji ni kubwa, nimeamua kutumia kidogo nilichonacho kujenga kisima chenye uwezo wa kuhudumia watu 3500 katika shule ya msingi eneo la Golani Kimara.
Wananchi wa huku wamekua wakipata shida ya maji sana na wenye uwezo wamekua wakinunua ndoo moja kwa tsh 1000, ambayo ni bei kubwa kugharamikia maji.
Hili ni tatizo kwakweli, sio hapa tu bali maeneo mengi nchi nzima.
Nimeona niwashirikishe jambo hili wapendwa wangu wote kwakua tuna nafasi ya kusaidia hata kama kidogo ila naamini “even a penny can change the world”
Ukitoa kidogo na mwingine pia akatoa basi lazima kutakua na mabadiliko
Tunaweza kuanza kufanya na kubariki maisha ya wanaotuzunguka kidogo kidogo
Tuanze leo.
Maji ni haki ya kila binadamu.
Lets save lives,help bring water”-Wolper on Instagram,

HONGERA SANA WOLPER, MUNGU AKUZIDISHIE MOYO WA HURUMA

 

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Hi there!

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364