-->

Wolper: Ufundi Unanilipa

MSANII wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper, amesema mbali na sanaa yake hiyo, amekuwa akipata hela nzuri kupitia kazi yake ya mitindo ambapo sasa ameamua kuwa fundi seremala.

Jacqueline Wolper

Wolper amesema huu ni wakati wake wa kutengeneza fedha ili kutimiza ndoto zake za kuishi maisha aliyojipangia tangu akiwa mdogo.

“Hakuna asiyependa maisha mazuri na tutambue tu hayaji kirahisi zaidi ya kujituma usiku na mchana kuhakikisha unaweka mambo yako sawa, sasa hivi nimewekeza zaidi kwenye mitindo na kama mnavyoniona kazi yangu ya useremala inanilipa sana, nashukuru Mungu hiki ninachokipata,” alisema Wolper.

“Unatakiwa upende hela yako, usitambe na hela ya mwanamume, usitambe na hela ya kupewa, fanya kazi yako ikupe heshima,” amesisitiza Wolper.

 

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364