VIDEO: Aliyeliombea gari lisichukuliwe na maji awa gumzo mitandaoni
Video moja inayomwonyesha mkazi wa Morogoro Bw. Nyangusi Laiser akiwa anaombea gari lake aina ya Toyota Land Cruiser lisichukuliwe na mafuriko, liligeuka kuwa burudani kwenye mtandao baada ya kusambaa sana kwenye mtandao.
Bw Laiser aliandika kwenye ukurasa wake wa Fesibuku siku ya Jumanne, ambapo tukio lilitokea, kwamba alikuwa kwenye gari na mke wake pamoja na kaka yake siku hiyo wakielekea shambani. Wakakwama na gari kwenye njia ya maji. Wakiwa wanahangaika kulitoa, dk 45 hivi, mvua ndogo ikaanza kunyesha. Bw Laiser akawashauri wenzake wakakinge mvua nyumba ya karibu. Lakini maji yakaanza kuongezeka kwa kasi.
Bw Laiser anasikika akiwa anaomba kwa nguvu, akimkemea shetani asichukue gari lake. Aliiambia MCL Digital kwamba aliukumbuka andiko la kwenye Biblia kwenye Yeremia 33:3 lisemalo, ‘Niite name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua.
Mwisho wa siku, gari halikuchukuliwa na maji yakakauka kabisa. Bw Laiser ni Mratibu wa Mkoa wa Morogoro wa shirika la Tacaids.
Mwananchi