Young Killer Afunguka Ishu ya Joh Makini Kubebwa
Msanii wa rap Bongo Young Killer amemdiss msanii wa Hip Hop Joh Makini kwenye ngoma yake mpya SINA SWAGA akidai kwamba anabebwa kisanaa.
Akiongea kupitia eNEWZ Killer amesema aliamua kuwakilisha baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakiongelewa na wasanii wengi ikiwemo Chid Benz ambaye aliongelea kwenye media na kutunga mistari inayoelezea jinsi gani Joh anabebwa kisanaa.
Hata hivyo Killer amesema kuwa kuna ushaidi mwingi wa picha kwenye blog tofauti zinazoonesha jinsi Joh anavyotuhumiwa kubebwa kisanaa na kusema hana tatizo na Joh hata akikutana naye atamsalimia kwa kuwa hayo maneno ya kubebwa yeye kayawakilisha tu kutoka kwa watu wengine ingawa yeye anamkubali.
eatv.tv