-->

JB Amvuta Muigizaji wa Zambia ‘Cassie’

Msanii mkongwe wa filamu na Mkurugenzi wa Jerusalem Film Company, Jacob Stephan ‘JB’ amemvuta muigizaji maarufu wa Zambia Cassie Kabwita kwa ajili ya kushiriki katika tamthilia yake mpya ya runinda iitwayo Jirani.

King Cassie tayari ameshashiri filamu ya ‘Vita Baridi’ pamoja na ‘Mzee wa Swagga’ akiwa na JB.

Wiki hii JB alikutana na muigizaji huyo na kuandika ujumbe huu,

“Jana nilikutana na @king_cassie1 mwigizaji toka zambia..ambaye tumewahi kushirikiana nae kwenye movie za..vita baridi na mzee wa swagga..Tuliongea mengi lakini kubwa ni kuwa atashiriki kwenye Tamthilia yetu nyingine..JIRANI..tutakayo anza kuishoot Mwezi wa pili…karibu tena jerusalem films cassie..navutiwa sana na uigizaji wako,”

Kwa upande wa muigizaji huyo aliiambia Bongo5, “Ine me supper excited Just gotten a lead role in a new TV series in Tanzania called JIRANI,”

Muigizaji huyo ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu, ameshinda tuzo mbalimbali za uigizaji ndani ya nchi yake pamoja na kimataifa.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364