Young Killer Afunguka Kuhusu Kufanya Kazi na Wasafi
Msanii Young Killer Msodoki amefunguka kuhusu suala la yeye kujiunga na lebo ya WCB, na kuwataka mashabiki watambue kuhusu ukweli wa suala hilo.
Akiongea kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV na kutolea ufafanuzi picha aliyopiga na Diamond na kuibua tetesi hizo, Young Killer amesema yeye ni msanii hivyo iwapo kutakuwa na haja ya kufanya nao kazi WCB, hatosita kwenda.
“Naomba ifahamike hivi, mimi ni msanii, hivyo WCB nikihitajika kufanya nao kazi, nitaenda kufanya nao kazi, ila si kweli nipo WCB, ile picha ilipigwa tu kama picha zingine ikapostiwa”, alisema Young Killer.
Hivi karibuni kuliibuka tetesi kuwa msanii huyo anatarajia kusainiwa na lebo ya WCB, baada ya kusambaa picha akiwa na bosi wa lebo hiyo, Diamond Plutnumz.
eatv.tv