Zari Awapa Makavu Wabaya Wake
Ni muda mrefu mahusiano ya Diamond na Zari yameelezwa kutokuwa mazuri kutokana na muimbaji huyo kuhusishwa kutoka na warembo wengine.
Kuna tetesi nyingi sana zimevuma kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni zikiwahusu Diamond na Zari.
Huku tetesi hizo zikimhusisha Diamond kusaliti mahusiano yake kwa kutoka na warembo wengine akiwemo Hamisa Mobetto na mrembo aliyetumika kwenye video ya wimbo wa ‘Kwetu’, Irene.
Kupitia mtandao wa instagram wa Zari ameandika ujumbe unaoonekana kuwalenga watu wanaomfuatilia na wasioyatakia mema mahusiano yao. “When your self made, it’s hard to break you no matter how hard they may try. I made me and the only person that can break me is ME not anybody. Ladies now wear this crown? and put them heels? on and keep it moving. Good night?,” ameandika Zari.
Hata hivyo wawili hao wanatarajia kupata mtoto pili wa kiume muda wowote kuanzia mwezi Disemba mwaka huu.
Bongo5