-->

ZIFF Yaanza Kupokea Maombi ya Wasanii

TAMASHA la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), limeanza kupokea maombi ya wasanii wa sanaa mbalimbali kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika kwa ajili ya ushiriki katika tamasha hilo kubwa.

ZIFF.-PR.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Profesa Mahando, maombi hayo yanatumwa kabla ya Machi 31, 2016 na yatumwe kupitia ‘YouTube link’, ‘Vimeo, Sound Cloud’, yakiambatanishwa na picha ya washiriki na maelezo yao yatumwe kupitia  HYPERLINK “https://us-mg5.mail.yahoo.com/neo/b/compose?to=mpa@ziff.or.tz” \t “_blank” mpa@ziff.or.tz.

Tamasha hilo kubwa kwa Afrika Mashariki, linalojumuisha maonyesho ya filamu, muziki na sanaa mbalimbali likiwa na lengo la kuwaleta watu wa mataifa mbalimbali pamoja, linatarajiwa kuanza Julai 9 hadi 17 likiwa na kaulimbiu ya ‘Ndiyo hii Safari Yetu’.

Katika siku hizo 10 za Tamasha hilo kazi mbalimbali za sanaa na utamaduni, filamu, muziki wa moja kwa moja na ule utakaochezwa na madjas utafanyika ili kuendelea utamaduni wa burudani katika tamasha hilo litakalofanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe, Stone Town visiwani Zanzibar.

Baadhi ya wasanii waliowahi kushiriki katika tamasha hilo ni Sarafina na Dorothy Masuka kutoka Afrika Kusini, Habib Koite na Mousa Diallo kutoka Mali, Grace Matata, Weusi, Yamoto kutoka Tanzania na wengine wengi kutoka mataifa mbalimbali.

Mtanzania

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364