Picha: Wachezaji wa DR Congo Watuzwa Magari ya Kifahari
Rais wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Laurent Kabila ameamua kuwazawadia magari wachezaji wa timu ya taifa ya Kongo walioshinda Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN), Rais Kabila ameagawa magari kwa wachezaji 23 na viongozi 7 waliofanikiwa kutwaa Kombe la CHAN kwa mwaka 2016, michuano ambayo imefanyika Rwanda.
DR Congo ilifanikiwa kuifunga timu ya taifa ya Mali kwa goli 3-0, na kutwaa taji lake la pili la michuano hiyo, baada ya kufanya hivyo kwa zaidi ya miaka minne nyuma, gari hizo walizopewa wachezaji wa timu ya taifa ya Kongo BBC inataja kuwa zinathamani ya KSH milioni 6 za Kenya kwa Tanzania ni Tsh Milioni 130 kwa kila gari. Michuano ya CHAN ilikuwa inashirikisha timu 16.
Millard Ayo