-->

Nay Ampiga Changa Director Wake

Muongozaji wa video kutoka Bongo, Nicklass, ambaye amefanya video ya ‘Shika adabu yako’ ya Nay wa Mitego alipigwa changa la macho na Nay juu ya video hiyo.

Nicklass

Akizungumza na Enewz Nicklass alisema kuwa Nay alimdanganya kuwa afanye video na wote aliowadis amekwisha ongea nao na haitakuwa na shida lakini kumbe haikuwa hivyo.

“Nay alivyokuja kunitaka tushuti video ya hiyo nyimbo, awali niligoma kwasababu ya dis alizozifanya lakini baada ya kunieleza kuwa ameshazungumza na wahusika waliokuwa wameimbwa katika nyimbo hiyo ikanibidi nikubali”, alisema Nicklass.

Lakini pia Nicklass, alizungumzia kipande ambacho kilileta utata katika video hiyo ambacho kilikuwa kikionesha kuwa dongo kwa mwanamuziki Shetta, Nicklass amesema kuwa karibia watu watatu walikataa kushuti kipengele hicho kutokana na uhusika wenyewe.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364