-->

Wabogojo aanika maisha ya Jack jela

Mkali wa mchezo wa sarakasi Bongo, Athumani Ford ‘Wabogojo’ anayefanya kazi za sanaa nchini China, amefunguka mambo kadhaa ya mwanamitindo Jacqueline Cliff ambaye amefungwa nchini humo kwa kosa la kukamatwa na madawa ya kulevya.

Wabogojo ambaye amekuja Bongo kwa ajili ya mapumziko mafupi, alisema kuwa mrembo huyo anaendelea vizuri sana gerezani na ni mtu ambaye ameshazoea hali ya huko na amekubaliana na ukweli halisi na amezidi kuwa mrembo tofauti na watu wanavyodhani.

“Kitu kizuri sana ni kwamba Jack yuko vizuri sana, amezidi kuwa mrembo maana wengi wanajua mtu ukienda jela ni kuchakaa tu lakini siyo kwa Jack kwa sababu ameshakubaliana na yalitokea, ananawiri,” alisema Wabogojo.

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa, kwenda kwake gerezani mara kwa mara, kunamfanya mrembo huyo kujisikia vizuri sana na kujiona kama yuko nyumbani na mara nyingi hapati muda wa kuwaza mambo ya huzuni kutokana na kifungo hicho.

“Hakuna kitu anachofarijika Jack kama akiniona pale, anapata faraja ya ajabu sana na mimi nitakuwa nafanya hivyo mpaka muda wangu wa kuishi nchini humo uishe kwa sababu hata mimi najiona fahari kutenda hivyo,” alisema Wabogojo.

Katika barua yake ya hivi karibuni aliyowaandikia Watanzania akieleza hisia zake na maisha yake kwa ujumla, Jack aliwashukuru watu wanaomtembelea gerezani akiwemo Wabogojo.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364