-->

Barnaba Unanikimbia Huniwezi – Linex

Msanii Linex amempa za uso msanii mwenzake ambaye naye ana sauti tamu ya kuimba Barnaba Clasic, na kusema kuwa anamuogopa kufanya naye kazi kwani kwa vyovyote vile atamfunika.

Linex-1

Kwenye ukurasa wake wa instagrama Linex ameandika akimtaka Barnba asikimbie wanapotakiwa kufanya kazi ya pamoja, kwani kila akimwambia anamkimbia.

“Mara ngapi wametokea wadau na wakawa tayari kuweka pesa zao mimi na wewe tufanye kitu Barnaba classic na ukawa unakimbia kimbia, uko talented na najua we pia unapenda ninachokifanya sasa kuna sababu gani ya we kuleta janja nyani kila tukipanga kufanya kazi?” aliandika Linex.

Linex ameendelea kuandika “Nikwambie kitu najua we ni msanii mzuri but usije kurogwa kukutana na mimi kwenye wimbo utai love Show, endelea kurun away shame on you Barnaba classic na uclasic wako”,

Kwa upande wake Barnaba ameonekana kumjibu Linex na kusema kuwa hajamkimbia siipokuwa thamani ya muziki wake hauna dau kwani kwake ndio chakula.

“Nakushangaa sana mzee Linex unapoleta hadithi za mimi kukimbia mzee kweli wewe!! Mimi nikukimbie au wewe umekimbia uwezo mzee.! kingine nataka nikwambie wewe Linex Sunday Mjeda, najua unapenda sana nyimbo zangu na pia uwa unapata baadhi ya line mbili 3 zinazokusaidia ndugu yangu alafu mwambie mdau aweke dau nililosema mimi sio wewe, na kwanza mimi sinaga dau mana muziki kwangu ni chakula sasa sikusomi mzee……..esus is my Power”, aliandika Barnaba.

EATV.TV

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364