-->

Mapokezi ya Richie Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalim JK Nyerere Jana Usiku

Richie akiwa na Katibu wa Bodi ya Filamu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalim JK Nyerere.

Richie akiwa na Katibu wa Bodi ya Filamu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalim JK Nyerere.

USHINDI huwa ni chachu kwa kila ashindaye hayo yamejitokeza leo usiku baada ya watayarishaji waliokuwa Naijeria kuingia mnamo saa saba kasoro wakiwa na mshindi mmoja aliyeshinda tuzo ya kipengele cha Filamu ya Lugha ya kigeni.

Amil shivji simon mwakifwamba

Mwakifwamba na Amili

Single mtambalike

Keki Richie danga

Single matambalike

Richie akiwalisha wanaye keki

Single Amil

Amil, Honeymoo na Richie shampen

Single Matambalike , kulwa kikumba

Dude akila Keki

Jacob stephen ,single matambalike

Jb akilishwa keki

Mwakifwamba, mtambalike

Richie akiongea na rais wa TAFF Mwakifwamba

Mshindi ambaye ni Single Mtambalike ‘Richie’ kupitia sinema ya Kitendawili, kitu kikubwa na cha kujivunia kabisa ilikuwa ni umati wa watu waliojitokeza kuwapokea mashujaa wetu ambao waliwakilisha Tanzania katika tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA 2016).

Usiku huu mashujaa waliopokelewa ni Staford Kihore, Amli Shivji, Honeymoon Aljabri, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ na Single Mtambalike ‘Richie’ waliingia usiku huo wakiwa na ndege ya shiriki la Ndege la Kenya KQ.

Uwanjani ngoma zilitawala na kuchangamsha wasanii wakicheza na kufurahia ushindi wa Swahilihood baada ya Richie kushuka na tuzo yake Lulu kwa amebaki huko akijaribu kufanya maongezi na watayarishaji wakubwa kwa kazi zake za mbele.

Pamoja na familia za wahusika lakini walikuwepo wasanii nyota kama Jacob Stephen ‘JB’, Kulwa kikumba ‘Dude’ Mzee Chilo, Niva, wakiongozwa na Katibu wa Bodi ya Filamu na Rais wa shirikisho la filamu (TAFF) waliowapongeza washindani wote.

Walikata keki nzuri kabisa pamoja na kufungua shampeni ilikuwa ni furaha na siku ya kihistoria katika tasnia ya filamu pamoja na kuwa usiku mkubwa lakini wasanii hawakuwa nyuma kuonyesha furaha yao.

Ripoti na Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364