Van Vicker Anaamini Tanzania Itapasua Zaidi, Lakini…
MUIGIZAJI nyota wa Ghana, Joseph van Vicker, amesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kuendelea kutamba baada ya wasanii wake wawili kushinda tuzo.
Single Mtambalike ‘Rich Rich’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ wameibuka washindi katika African Magic People’s Choice Awards zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Eko kwenye Kisiwa cha Victoria jijini hapa, juzi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Van Vicker alisema Tanzania kuna vipaji ambavyo vinaweza kuendelea kutamba.
“Tanzania inajulikana kuwa ni moja ya nchi za Afrika zinazoweza kufanya vizuri na leo ni mfano mzuri,” alisema.
Chanzo: GPL