Abdul Kiba Atolea Ufafanuzi Kuhusu Kujiunga na WCB Wasafi
Staa wa Bongo Fleva, Abdul Kiba ametolea ufafanuzi kuhusu taarifa iliyosambaa mitandaoni kujiunga na WCB WASAFI ambayo inamilikiwa na Diamond Platnumz.
Akiaongea na cloudsfm.com Abdul Kiba ambae ni mdogowake na msanii Abdul Kiba alieleza.
‘’Ni kweli nilizungumza hiyo lakini wengi wao waliitafsiri vibaya kauli yangu kwasababu ukizungumzia mtonyo nilimaanisha kwamba nina uwezo wa kufanya nao kazi aidha ikitokea labda ‘featuring’ au kuna shoo naweza nikashirikiana nao kwa sababu ni mkataba utatakiwa upite hapo then pesa imwagike nifanye nao kazi ila siku maanisha kwamba nina uwezo wa kuhama ‘lebo’ kutoka hapa nilipo kwenda kwao, nadhani wengi wao waliipokea kauli yangu vibaya’
Kuiona Video ya Abdul Kiba Bayoyo – Bofya hapa