-->

Afya ya Chid Benz Yawashtua Wengi

Kuna picha siku ya jana zilikuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Chid Benz akiwa amepungua mwili na kuonekana ni dhaifu, jambo ambalo limewahuzunisha mashabiki wengi na wadau mbali mbali, huku wengine wakisema kuwa Chid Benz anahitaji msaada kwani hali yake ni mbaya.

CHID benzi

Kwa upande wake msanii Afande Sele alipost picha hiyo ya Chid Benz na kusema madawa ya kulevya ambayo yanaingia nchini yanaua masela wa leo na hayaleti maendeleo yoyote zaidi ya kupoteza vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa la leo.

“Yanapita kwa njia gani madawa ya kulevya hapa nchini? anayasambaza nani mitaani kote? madawa ya kulevya hayaleti maendeleo, madawa ya kulevya yanaua masela leo” Afande Sele

Kwa upande wake mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe amesema mambo yaliyokea kwenye mpira leo (Jana) siyo ya kushangaza sana kama hali ya Afya ya msanii Chid Benz inavyoshangaza na kudai kuwa msanii huyo asiendelee kujidanganya anahitaji msaada mkubwa wa haraka, pia amewataka marafiki wa msanii huyo wasiendelee kumdanganya Chid Benz kwani hali yake ni mbaya.

“Yaliyotokea katika mpira leo sio ya kushangaza sana kuliko hali ya afya ya CHID BENZ… Anahitaji msaada wa haraka sana..asiendelee kujidanganya tena, na hata rafiki zake wasiendelee kumdanganya tena….SO SAD”. Alimalizia Edo Kumwembe

Siku kadhaa zilizopita Chid Benz akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio alisema kwa sasa anatambua alipotoka na alipo sasa kauli ambayo ilionyesha kujutia mambo ambayo yamempelekea kufika katika hatua hiyo.

aFANDE

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364