-->

Khadija Kopa Adai Umri Unamtupa Mkono, Ajipanga Kuacha Kuimba

p>Malkia wa muziki wa taarab nchini, Khadija Kopa amesema kwa sasa anajipanga kuwekeza zaidi kwenye biashara kwa kuwa umri wa kuimba unamtupa mkono.

KHADIJA KOPA

Akizungumza katika kipindi cha Uhondo cha EFM Ijumaa iliyopita, Khadija amesema moja ya biashara kati ya zile ambazo anatarajia kuzifungua ni mgahawa.

“Hivi sasa nampango wa kufungua mgahawa mkubwa, nataka nifungue na duka langu moja kubwa.” alisema Khadija “Kwa hiyo nataka kufanya biashara kusema ukweli kwa sababu sasa hivi na umri mkubwa, na watoto wangu wameshaanza kuimba, kwa hiyo naona utafika wakati mimi hata poda haitakaa usoni kutokana na makwinyanzi, kwa hiyo nitahitaji muda wa kupunzika, niwapishe watoto wangu ambao naona kuna wengine watakuwa wakubwa hata zaidi yangu,” aliongeza.

Pia Khadija Kopa amesema kwa sasa hivi angekuwa mbali zaidi kibishara lakini tukio la kufiwa na mume wake limemrudisha nyuma.

Bongo 5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364