-->

Afya ya Mr. Nice Kuteteleka… Simulizi Yake Inasikitisha

SIKU chache baada ya kusambaa kwa picha yake inayomuonesha akiwa amepungua mwili na kuzua mjadala mitandaoni huku wengi wakimuonea huruma, mkongwe wa Muziki wa Takeu, Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ ameibuka na kufungukia afya yake.

MR-NICE1

Picha inayomuonesha Nice akiwa amepungua mwili ilizagaa mapema wiki hii kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliochangia mjadala wa picha hiyo, walisema staa huyo aliyetikisa kwa utajiri enzi hizo, kwa sasa atakuwa anaumwa sana huku mjadala mkubwa ukawa ni ya lini?

Baada ya Ijumaa kuinasa picha hiyo, lilifanya jitihada za kumpata msanii huyo kwa kumvutia waya alipopatikana, alifunguka kwa kirefu kuhusu afya yake:

“Kwanza hiyo picha ni ya kitambo sana. Si unakumbua lile sakata langu la mimi kulishwa sumu kwenye chakula? Basi ndiyo kipindi kile.

“Namshukuru Mungu niliiwahi ile sumu na kupewa dawa ambazo natumia mpaka sasa. Kweli nilipungua lakini ni wakati huo, kwa sasa sipo hivyo kama kwenye hiyo picha inayosambazwa mitandaoni,” alisema Mr. Nice.

Akaongeza kuwa ni kweli afya yake haiko poa sana kwa kuwa bado anaendelea kutumia dawa za kuimaliza sumu ile lakini siyo kama vile anavyoonekana kwenye picha hiyo.

Chanzo: GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364